WAPENI MISAADA WANAWAKE WALIOPO MAHABUSU - Rhevan Media

WAPENI MISAADA WANAWAKE WALIOPO MAHABUSU



Dar es Salaam. Watanzania wanaopenda kutoa misaada wamekumbushwa kuwasaidia wanawake wanaoshikiliwa kwenye vituo vya polisi.
Rai hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Inspekta Prisca Komba kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa British Council jijini hapa.
Inspekta Komba alisema mahabusi wanawake hupata wakati mgumu vituoni hasa wanapokosa huduma muhimu kama taulo za kike, sabuni na nguo za kujistiri.
“Vituo vya polisi havina kitu ndiyo maana nasisitiza watu wajitoe kusaidia hasa kwa upande wa wanawake.Tunahitaji taulo za kike, sabuni na nguo za kuwastiri,” alisema.
Balozi wa Uingereza, Sarah Cooke alisema Serikali yake itaendelea kusaidia elimu kwa watoto wa kike kama njia pekee ya ukombozi wao.
“Najivunia, Serikali yangu imekuwa mstari wa mbele kusaidia elimu kwa wanawake na watoto wa kike, masuala yote yanayomgusa mwanamke kwetu ni kipaumbele,”alisema Cooke.







Previous
Next Post »