WAGONJWA 700 KUFANYIWWA UPASUAJI WA KIFUA JKCI - Rhevan Media

WAGONJWA 700 KUFANYIWWA UPASUAJI WA KIFUA JKCI



Dar es Salaam. Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imejipanga kufanya upasuaji wa kifua kwa wagonjwa 700 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 1,000 kwa kutumia mtambo wa Catheterization ndani ya mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa Operesheni JKCI, Dk Bashiri Nyangasa amesema nia ya kufanya hivyo ni kutaka kuhakikisha kuwa matatizo ya moyo yanapungua hapa nchini.
"Tusipofanya hivyo tutakua katika hatari ya kuongeza vifo vya wagonjwa wanaoongezeka siku hadi siku kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na mabonanza mbalimbali," alisema Dk Nyangasa.

Previous
Next Post »