Uwasilishwaji wa taarifa hizo ni kwa mujibu wa vifungu vya 73 (1) na 73 (2) vya sheria ya fidia kwa wafanyakazi sura ya 263 marejeo ya mwaka 2015 kinachomtaka kila mwajiri kuwasilisha taarifa hizo kabla ya tarehe 31 ya mwezi Machi kila mwaka.
Kwa tangazo hili, nawataarifu waajiri wote kuwa uwasilishwaji wa fomu hizo ni kwa kutumia fomu WCR-3 na mwisho wa kuziwasilisha ni tarehe 31.03.2017.
Fomu zilizojazwa kikamilifu ziwasilishwe kwenye ofisi za Mfuko zilizopo ghorofa ya 6, Jengo la GEPF House, Kitalu na 37, Regent Estate, Barabara ya Bagamoyo au Ofisi za Kazi zilizopo mikoani na wilayani Tanzania Bara.
Aidha, fomu WCR-3 inapatikana kwenye tovuti ya Mfuko www.wcf.go.tz, Makao Makuu ya Mfuko au kwenye Ofisi za Kazi zilizopo mikoani na wilayani Tanzania Bara. Kwa mawasiliano zaidi piga simu za bure 0800110028 au 0800110029.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
Kitalu na. 37, GEPF House, Barabara ya Bagamoyo, Regent Estate, Ghorofa ya 6.
S.L.P 79655,
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
Kitalu na. 37, GEPF House, Barabara ya Bagamoyo, Regent Estate, Ghorofa ya 6.
S.L.P 79655,
Simu: +255 22 2926107, +255 22 2926108,
Nukushi: +255 22 2926109,
Nukushi: +255 22 2926109,
Sign up here with your email
