Dk. Gudila Valentine akiwasilisha mada kuhusu ugonjwa wa Figo katika kongamano la kitaaluma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Figo Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 9.
Baadhi ya Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali kuhusu magonjwa ya Figo zilizowasilishwa katika kongamano hilo leo .
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimuhudumia mgonjwa katika kitengo cha Figo, kushoto ni kiongozi wa kitengo hicho Sister Judith Mwaipopo na kulia ni Sister Lucy Kyombo.
……..
Watanzania wametakiwa kuepuka utumiaji holela wa dawa za maumivu ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa ya Figo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jakline Shoo alipokua akiwasilisha mada katika maadhimisha siku ya figo Duniani, katika kongamano la kitaaluma lililofanyika leo katika ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali hiyo.
Akifafanua Dk. Shoo amesema ni vema watu wakaepuka matumizi holela ya dawa za maumivu kwani ni chanzo cha magonjwa ya figo lakini pia kuepuka unene uliokithiri kwa kula mlo bora na kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ya Kisukari na shinikizo la damu ambayo yanachangia mtu kupata ugonjwa sugu wa figo.
Akielezea kuhusu wagonjwa wanaohudumiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Shoo amesema katika Kiliniki yao kwa kila mwezi huwaona wagonjwa watu wazima kati ya 120 hadi 150 .
Pia takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya watu Duniani tayari wanaugua ugonjwa sugu wa figo na kwamba inakadiriwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 70 ya wagonjwa watakua wanatokea katika nchi zilizopo Ukanda wa Jangwa la Sahara.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Figo Duniani mwaka huu ni ugonjwa wa figo na uzito uliozidi , mienendo bora ya maisha kwa ajili ya afya bora ya Figo.
Sign up here with your email