
Ubalozi wa Uswisi nchini umekutanisha wananchi mbalimbali kuzungumza kuhusa haki za binadamu kwa jinsi gani zinatekelezwa Tanzania na kimataifa na kuangalia jinsi gani kila mtu kwa nafasi yake anaweza kushiriki kuzilinda.
Pamoja na kuzungumza kuhusu haki za binadamu pia walizungumza kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii ambapo washiriki walipata nafasi ya kutoa mawazo yao na wengi wao wakionekana kutofahamu haki zao za kimsingi na jinsi gani wanaweza kuzidai.
Akizungumza na MO Blog mmoja wa washiriki wa mdahalo huo, Mkurugenzi wa Uangalizi wa Haki za Binadamu na Uwajibikaji kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hilda Urio alisema changamoto kubwa ambayo ipo kwa sasa ni wananchi kutofahamu haki zao na mfumo ambao unatumika nchini.
“Haki za binadamu nyingi na za muda mrefu na kuna mikataba ya kimataifa ambayo sheria zake huingia katika katiba ya nchi, na ni muhimu kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusu haki za binadamu ili watu waweze kuzifahamu,
“Tatizo lililopo sasa hivi ni tatizo la kimfumo, mfumo uliopo sasa hivi bado unachangamoto ya kuweka usawa wa upatikanaji wa fursa lakini pia upatikanaji wa haki kwa wanawake na wanaume, ipo nafasi kwa asasi za kiraia na wadau mbalimbali kutoa elimu na kuhakikisha haki hizi zinalindwa,” alisema Urio.
Balozi wa Uswisi nchini, Florence Mattli akifungua mdahalo huo.
Mwongozaji wa mdahalo, Mkurugenzi Mkazi wa BBC Media Action nchini, Colin Spurway akiwakaribisha washiriki.
Mkurugenzi wa Uangalizi wa Haki za Binadamu na Uwajibikaji kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hilda Urio akizungumza katika madahalo ulioandaliwa na Ubalozi wa Uswisi nchini ukijadili Haki za Binadamu.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Tume ya Haki za Binadamu, Nabor Assey akichangia mada kuhusu Haki za Binadamu katika mdahalo ulioandaliwa na Ubalozi wa Uswisi nchini.
Washiriki wakitoa maoni yao kuhusu utekelezwaji wa Haki za Binadamu nchini na kimataifa.




Sign up here with your email
