Rwanda yamteua Mjerumani kuongoza timu ya taifa.
Kocha Antoine Hey kutoka Ujerumani ametangazwa na chama cha soka cha Rwanda FERWAFA kuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Amavubi na ametia kandarasi ya miaka 2.
Antoine Hey amewashinda Mswizi Raoul Savoy na Mreno José Rui Lopes Águas .
Timu ya taifa ya Rwanda ilikuwa bila mkufunzi tangu kutimuliwa kwa Jonny McKinstry kutoka Ireland ya Kaskazini mwezi wa 8 mwaka jana.
Antoine Hey mwenye umri wa miaka 46 aliwahi kufundisha timu za mataifa ya Lesotho, Gambia, Liberia na Kenya.
Sign up here with your email