SHAKA AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA MAKATIBU WILAYA NA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,SONGWE,KATAVI,RUKWA,KIGOMA NA TANGA - Rhevan Media

SHAKA AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA MAKATIBU WILAYA NA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,SONGWE,KATAVI,RUKWA,KIGOMA NA TANGA


Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa kwanza Kulia Akipeana Mikono na watendaji Mara Baada ya Kuwasili kufungua
semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe,
Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga,  iliyofanyika katika katika
ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwasili  katika
ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya kufungua
semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe,
Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.
Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana Wa Chama cha mapinduzi Ndg:Amani Kajuna akizungumza kumkaribisha Ndg:Kaimu katibu Mkuu  UVCCM Shaka Hamdu Shaka kufungua
semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe,
Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika
ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua
semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe,
Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika
ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
 Makatibu wakimsikiliza kwa Makakini
Akizungumzia
kuhusu mabadiliko ya katiba CCM na kanuni za jumuiya  amewahimiza
watendaji hao kutopindisha na kupotosha katika eneo lolote badala yake
 wafanye kazi ya kuelimisha na kusimamia utekelezaji wake.
Amesema mabadiliko  ya katiba ya CCM kimsingi yameonyesha njia,  mweleko na dira ya chama katika kujimarisha kisiasa.
*”Mabadiliko
Katiba ya CCM na kanuni za jumuiya hayakuzuka kama mvua za vuli
 yamefanyiwa upembuzi yakinifu, tathmini za kitaalam katika taaswira ya
sayansi ya siasa, yakitekelezwa kwa kufuata misingi yake, CCM itaendelea
kupeta miaka   mia mbili ijayo “Alisema*
Akizungumzia kuhusu uchaguzi Wa ndani ya  chama na jumuiya alisema.
*”Lazima
 mkumbuke ninyi ndio wakurugenzi wa  uchaguzi wa UVCCM katika maeneo
yenu   msiende kusimamia  chaguzi mkiongozwa na utashi na visasi,
fuateni kanuni, taratibu ili kuzifanya chaguzi zetu kuwa huru, za  haki
 na za wazi,  nawakumbusha  wakati wote pendeni kuishi katika matamshi
na maelekezo  ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt Magufuli “Alisisitiza* 
Aliwakumbusha
watendaji hao wa jumuiya kuwa  watakuwa na jukumu kupitia vikao vyao
vya kikatiba na kikanuni  kuchuja na kuwapima wagombea kwa vigezo
stahili na si kuzoazoa watu ambao hawatokani na jumuiya wala CCM.
Kuhusu
Mali za jumuiya alisema UVCCM imeamua kuandaa semina hiyo kuwajengea
uwezo  watendaji katika masuala ya uchumi na biashara, namna ya kuibua
miradi mipya, kuandaa maandiko ya miradi na usimamizi  ili iwe endelevu,
 namna ya kutumia fursa zilizopo kuweza kuongeza kipato cha jumuiya na
 kuwatoa katika ombwe la  kujiona hawezi kuendesha jumuiya  bila kuomba
omba.
*”Nendeni mkabuni,
 mkatunze na kulinda Mali za jumuiya ili zinufaishe taasisi
hatutamvumilia mbadhirifu au mhujumu wa mali au kutumia mamlaka yake
 vibaya katika kusimamia mali hizo, hata  mimi ikibainika  pako pahala
nimekiuka taratibu au maelekezo kwa makusudi  niko  tayari kuwajibika
 ili kulinda heshima na nidhamu ya Mali zetu  tunahitaji kuiona UVCCM
mpya si kwa maneno tena  bali ni  kwa vitendo”*
Kaimu
Katibu Mkuu aliwataka vijana wote nchini kumuunga mkono Mwenyekiti wa
CCM na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe  Magufuli
kwani amekuwa akipigania maslahi ya umma, kujenga uchumi imara, kutetea
haki na ujenzi wa demokrasia  endelevu .
Previous
Next Post »