RAIS WA BENKI YA DUNIA AWASILI NCHINI KUSHIRIKI KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA BARABARA ZA JUU UBUNGO. - Rhevan Media

RAIS WA BENKI YA DUNIA AWASILI NCHINI KUSHIRIKI KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA BARABARA ZA JUU UBUNGO.

dun1
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Mshauri Mwandamizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia nchi 21 Kanda ya Afrika Bw. Wilson Toninga Banda, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim.
dun2
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akipeana Mkono na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bi. Bella Bird, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim.
dun3
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bella Bird na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa nchi ya Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi Bw. Andrew Bvumbe (katikati) wakifurahia jambo wakati  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim akisubiriwa kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
dun4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akipeana Mkono na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
dun5
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akimuongoza  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim (kulia) kwenda katika eneo aliloandaliwa ili kufanya mazungumzo mafupi  baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
dun6
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na  Rais wa Benki ya Dunia  Dkt. Jim Yong Kim (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
dun7
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa kwenye mazungumzo mafupi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
dun8
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa kwenye mazungumzo mafupi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
dun9
Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), na maafisa wengine wa Serikali walipo wasili katika moja ya Hotel jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
………………………………………………………………………………
Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Akiwa hapa nchini, Dkt. Jim Yong Kim, atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar Es Salaam siku ya Jumatatu, tarehe 20 Machi 2017 ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia utekelezaji wa miradi mikubwa inayotarajiwa kutekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia katika ma kisha watashiriki uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara za Juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange) jijini Dar es salaam.
Aidha, Rais Magufuli na mgeni wake watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba mitatu;  wa kwanza ukiwa ni Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa mabasi yaendayo haraka-DART, pamoja na ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Ubungo (Dar es Salaam Urban Transport Project (DUTP);
Mkataba wa pili utakuwa ni kuanza kwa Awamu ya pili ya mradi wa Uboreshaji wa Upatikanaji wa Maji safi na uboreshaji wa miundombinu ya maji taka (Water and Sanitation Project) huku mkataba wa tatu ukiwa ni wa Uboreshaji wa Miundombinu na Huduma za msingi katika baadhi ya miji (Tanzania Strategic Cities Project).
Wakati wa ziara hiyo, Dkt. Kim atapata pia fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Zanaki iliyopo Manispaa ya Ilala, ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha elimu ya msingi unaofadhiliwa ma Benki hiyo
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais huyo wa Benki ya Dunia kuitembelea nchi ya Tanzania.
Imetolewa na Kitengo cha Mawsiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
19 Machi, 2017
Previous
Next Post »