Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi hawapo pichani kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.Sign up here with your email






