PLUIJM ATUA SINGIDA UNITED,AMSAJILI MZIMBABWE - Rhevan Media

PLUIJM ATUA SINGIDA UNITED,AMSAJILI MZIMBABWE


pluijm
Kuna msemo unasema ukisema cha nini,wenzako wanajiuliza watakipata Lini baada ya kutupiwa Virango na Mabingwa watetezi ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Wana jangwani Mholanzi Hans Van Der Pluijm hatimaye amejiunga na klabu ya Singida United iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Msimu ujao.
Inasemekana aliyekamilisha suala nzima la usajili wa Kocha huyu ni Mbunge wa Singida ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe.Mwigulu Nchemba na pia nimshabiki wa kutupwa wa klabu ya Yanga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu hiyo ambayo itakuwa inatumia uwanja Mkongwe wa Nafua uliopo Mjini Singida.
Ikumbukwe kuwa Mh.Nchemba alimrudisha Pluijm kwenye klabu ya Yanga baada ya kutangaza kuiacha timu hiyo baada ya tetezi za kuwa nafasi yake inakuja kuchukuliwa na Kocha wa sasa George Lwandamina na Mholanzi huyu alipandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo hata hivyo hakudumu kwenye nafasi hiyo ambapo alisitishwa Mkataba wake.
Pluijm amefundisha Yanga kwa awamu mbili tangu mwaka 2014 alipoanza kwa kufanya kazi kwa nusu msimu, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts kabla ya kwenda Uarabuni.
Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana. 
Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm  aliondoka baada ya kutofautiana na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.
Kabla ya kuhamishiwa kwenye Ukurugenzi wa Ufundi, Pluijm aliiongoza Yanga katika jumla ya mechi 128, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21.
Msimu uliopita ulikuwa mzuri zaidi kwake, akibeba mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 na mara ya pili kihistoria. Yanga ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998 kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Na kwa mafanikio hayo, haikuwa ajabu Pluijm akishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu uliopita.
Mapema wiki hii, Singida United ilimsajili kiungo Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn Fc ya Zimbabwe kwa mkataba wa miaka miwili. 
Singida United imerejea Ligi Kuu msimu huu baada ya msoto wa zaidi ya miaka 15 tangu ishuke Daraja.   

Previous
Next Post »