MAHAKAMA YAMNG'ATUA MAMLAKANI RAIS WA KOREA KUSINI - Rhevan Media

MAHAKAMA YAMNG'ATUA MAMLAKANI RAIS WA KOREA KUSINI

Rais wa Korea kusini aliyengatuliwa mamlakani na mahakama Park Guen HyeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Korea kusini aliyengatuliwa mamlakani na mahakama Park Guen Hye
Mahakama ya juu nchini Korea Kusini imeunga mkono uamuzi wa bunge wa kumuondoa rais wa taifa hilo Park Geun-hye mamlakani.
Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.
Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.
Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.
Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.
Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.
Rais huyo sasa amepokonywa uwezo wa kutoshtakiwa na sasa anaweza kusimamishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka.
Wapinzani wa Park Geun Hye walisherehekea uamuzi huo katika barabra za mji wa SeoulHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWapinzani wa Park Geun Hye walisherehekea uamuzi huo katika barabra za mji wa Seoul
Bi Park alikuwa amesimamishwa kuhudumu kama rais tangu mwezi Disemba huku waziri mkuu wa taifa hilo akichukua majukumu ya kuongoza taifa.
Bi Choi wakati huohuo ameshtakiwa kwa kuchukua hongo kwa madai ya kuyashinikiza makampuni makubwa kumpa pesa huku akiahidi kwamba kampuni hizo zitapendelewa na serikali.
Bi Park ameshtumiwa kwa kushirikiana na Choi.
Jopo la majaji wanane katika mahakama ya kikatiba liliangazia mashtaka yanayomkabili bi Park na kuamua kwamba kulikuwa na sababu mwafaka za kumwachisha kazi.
Wafuasi wa rais huyo walibubujikwa na mchazo baada ya uamuzi huo.Haki miliki ya pichaAP
Image captionWafuasi wa rais huyo walibubujikwa na mchazo baada ya uamuzi huo.
Makundi ya watu yalikuwa yemekongamana nje ya jengo la mahakama hiyo kusikiza uamuzi utakaotolewa swala ambalo limezua maandamano katika mji mkuu wa Seoul na miji mingine.
Mahakama iliamuru kwamba alitoa nakala nyingi za siri ikiwa ni ukiukaji wa kiapo alichokula cha kulinda siri za serikali mbali na kukiuka sheria kwa kumruhusu bi Choi kuingilia maswala ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
Previous
Next Post »