Hispania, Madrid. Mchezaji wa Real Madrid, Sergio Ramos amesema kwamba milango kwa timu hiyo ipo wazi kwa Kylian Mbappe ambaye amekuwa anahusisha kuhamia kwenye timu hiyo.
Mchezaji huyo raia wa Ufaransa anayeichezea Monaco, amekuwa gumzo Ulaya kutokana na kuonyesha kiwango cha juu kwenye mashindano ya Ulaya.
Mbappe (18) amekuwa kwenye mtego wa kila timu kubwa barani Ulaya zikiwamo Chelsea, Real Madrid, Barcelona na Manchester United.
Sign up here with your email