Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya Mbwawa katika mkutano wa adhara ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo
Mbunge huyo akisalimiana na mmoja wa wakinamama ambao ni wafanyabiashara ndogo ndogo katika soko dogo la Miswe
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akikagua mradi wa ujenzi wa choo kinachojengwa kwa ajili ya zahanati ya Miswe ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi(PICHA NA VICTOR MASANGU.
WANANCHI wa kata ya Mbwawa iliyopo katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mji mkoani Pwani wamelalamikia huduma mbovu zinazotolewa na wauguzi na madaktari wa zahanati ya Miswe na kupelekea wagonjwa kushindwa kupatiwa huduma ya matibabu kwa wakati hali ambayo inawalazimu baadhi yao kwenda kutibiwa katika maeneo mengine.
Malalamiko hayo yamekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kufanya ziara yake ya kikazi kwa wananchi wa kata ya Mbwewe kwa ajili ya kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyoibuiwa pamoja na kuweza kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananachi wake.
Wananchi hao akiwemo Theresia Mtatiro pamoja na Sudy Musa hawakusita kutoa kilio chao jinsi wanavyopata shida na usumbufu mkubwa katika suala la kupatiwa huduma ya matibabu inayostahili sambamba na kumwomba Mbunge kumchukulia hatua za kinidhani daktari wa zahanati ya Miswe anayefahamika kwa jina la Chacha Malwa kutokana na kuwanyanyasa wagonjwa bila sababu za msingi.
“Sisi kama wananchi wa kata hii ya Mbwawa kwa kweli tunapata shidasana katika huduma ya afya na zahanati yetu hii ya Miswe kwa kweli tukienda kwa ajili ya matibabu hata dawa wakati mwingine tunakosa vifaa tiba navyo ni shida, pamoja na hilo kuna daktari wetu anaitwa chacha sisi wananchi hatumtaki kabisa kumwona maana anatunyanyasa sana na lugha yake ni chafu,”walisema wananchi hao.
Katika hatua nyingine wananchi hao walisikitihswa na kuona zahanati hiyo siku nyingine za jumapili hawapati huduma ya matibabu na pindi panapofungwa ufunguo anakabidhiwa mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hivyo tunajikuta tunashindwa kupatiwa matibabu kama inavyotakiwa.
Kutokana na kuibuka kwa sakata hilo la malalmiko ya wananchi ilimlazimu Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kuinua mbele ya hadhara ya wananchi na kumuagiza Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya Mji kumwondoa na kumpeleka sehemu nyingine daktari wa zahanati hiyo ya Miswe kutokana na wananchi wa eneo hilo hawataki kumwona akiendelea na kazi katika sehemu hiyo.
Koka alibainisha kwamba serikali ya awamu tano ianyoongozwa na Rais Dr John Magufuli haiwezi kuwavulimilia watendaji ambao hawawezi kutimiza wajibu wao na badala yake itahakikisha inawachukulia hatua kali za kisheria endapo wakibainika kwanakwamisha juhudi za serikali katika kuleta chachu ya maendeleo.
“Wananchi wangu mmelalamika sana kwamba hampati huduma bora lakini mimi sasa namwagiza Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya mji kumwondo huyu Dr Chacha ambaye inaonekana amekuwa ni kero sana katika zahanati hii ya Miswe na mini haya yote nitamweleza Mkurugenzi wa mji hata mimi Mbunge simtaki aondoke,”alisema Koka.
Akijibu baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na wananchi katika mkutano wa adhara kuhusiana na mapungufu yaliyopo katika zahanati ya Miswe Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kibaha Amiry Lumumba aliwaomba wananchi wawe watulivu na kuhakikisha endapo wanachangamoto zoozte wasisiste kutoa taarifa mapema katika idara husika ili ziweze kufanyiwa kazi.
WANANCHI wa kata ya Mbwawa katika halmashauri ya Wilayaya Kibaha mji kwa sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na kukabiliwa na changamoto zinazoikabili zahanati ya Miswe hivyo kupelekea utoaji wa kuwahudumiwa wagonjwa kuzolota kwa kiasi kikubwa na kuwafanya wakati mwingine kutumia gharama kwenda kutibiwa katika maeneo mengine.
Sign up here with your email