KIMENUKA : TAARIFA ZA KODI ZA TRUMP ZA MWAKA 2005 ZAFICHULIWA - Rhevan Media

KIMENUKA : TAARIFA ZA KODI ZA TRUMP ZA MWAKA 2005 ZAFICHULIWA

Donald Trump akiwa White House. 13 Machi 2017Haki miliki ya pichaAP
Image captionBw Trump alikataa kufichua taarifa zake za malipo ya kodi
Rais wa Marekani Donald Trump alilipa kodi ya jumla ya $38m (£31m) kwa mapato yake ya $150m (£123m) mwaka 2005, taarifa za malipo yake ya kodi ambazo zimefichuliwa zinaonesha.
Taarifa ya kurasa mbili ya malipo yake ya kodi ilifichuliwa na runinga ya MSNBC ya Marekani, jambo ambalo limekera sana ikulu ya White House.
Maafisa wa ikulu wamesema ni kinyume cha sheria kuchapisha taarifa hizo.
Bw Trump alikataa kutoa taarifa zake za malipo ya kodi wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais, hatua iliyoenda kinyume na utamaduni wa wagombea urais nchini Marekani.
Taarifa hiyo ya kurasa mbili ni sehemu tu ya taarifa kamilifu ya malipo yake ya kodi na haina maelezo ya kina kuhusu mapato ya Bw Trump.
Hata hivyo, waandishi wa habari wanasema bado ni ufichuzi mkubwa ikizingatiwa kwamba ni maelezo machache sana yanayofahamika kuhusu ulipaji kodi wa Rais Trump na kwamba taarifa hizo mpya huenda zikamuongezea shinikizo za kumtaka afichue zaidi.
Taarifa hiyo inaonesha Bw Trump alilipa kodi ya $5.3m kwa serikali na kodi nyingine ya ziada ya $31m kwa kile kinachofahamika kama kodi mbadala ya chini (AMT).
AMT ilianzishwa miaka 50 iliyopita kuwazuia watu matajiri zaidi wasitumie mapengo mbalimbali kisheria kukwepa kulipa kodi.
Kodi hiyo ya $38m ni kwa kiwango cha 24%, kiwango cha juu kuliko kile cha raia wa Marekani wa kadiri.
Hata hivyo ni chini ya kiwango cha 27.4% ambacho kwa kawaida hulipiwa na watu wanaopata mapato ya juu.
Grey line
Ingawa ni kosa kisheria mtu kufichua taarifa za kodi, mtangazaji wa MSNBC Rachel Maddow alisema shirika hilo la habari lilitumia sheria ya Marekebisho ya Kwanza ya Haki za Kimsingi kuhusu haki ya kuchapisha habari kwa maslahi ya umma.
Mwanahabari David Cay Johnston, aliyehojiwa na MSNBC, alisema alipokea taarifa hizo kutoka kwa mtu ambaye hakutaka jina lake lifichuliwe.
Kupitia taarifa iliyotolewa kabla ya habari hizo kupeperushwa, White House ilisema: "Unafahamu kwamba unataka sana kuongeza idadi ya watu wanaokutazama pale unapofika hatua ya kuvunja sheria kupeperusha habari kuhusu taarifa ya kodi ya kurasa mbili ya mwongo mmoja uliopita."
Maafisa wa ikulu walisema Bw Trump alikuwa na wajibu wa kulipa kodi isiyozidi ile inayotakiwa kisheria.
Tangu mwaka 1976, wagombea urais wote wamekuwa wakitangaza hadharani taarifa zao za kodi, ingawa si hitaji la kisheria.
Donald Trump na Shinzo AbeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMiongoni mwa mali nyingine, Bw Trump humiliki viwanja vya gofu na hoteli za kifahari
Wakati wa kampeni za urais mwaka jana, mgombea wa Democratic Hillary Clinton katika mdahalo kati ya wawili hao, alimtuhumu Bw Trump kwa kutolipa kodi inayohitajika kisheria.
Bw Trump alimjibu: "Hilo basi linanifanya kuwa mtu mwerevu sana."
Oktoba mwaka jana, gazeti la New York Times lilifichua sehemu ya taarifa za kodi za Bw Trump za mwaka 1995 zilizoonyesha alipata hasara ya $916m (£753m).
Wachambuzi wanasema kuna uwezekano kwamba hilo lilimpa nafuu ya kutolipa kodi ya mapato kwa hadi miaka 18 baadaye.
Previous
Next Post »