Songea. Mtuhumiwa anayedaiwa kupatikana na meno ya tembo yenye thamani ya Sh500 milioni, Daudi Matola (41) mkazi wa Wilaya ya Namtumbo amekutwa amekufa akiwa mahabusu mjini hapa.
Anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia suruali aliyoifunga kwenye dirisha la choo cha mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Songea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji amesema tukio hilo lilitokea Machi 9 saa 9:55 usiku.
Mwombeji amesema inadaiwa siku ya tukio Matola akiwa mahabusu alienda chooni ambako alijinyonga kwa kutumia suruali yake.
Sign up here with your email