BAD NWES : MAMA MLEZI WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFARIKI DUNIA - Rhevan Media

BAD NWES : MAMA MLEZI WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFARIKI DUNIA


Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo.

Kupitia mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru jamii kwa salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri.

"Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo". Kauli ya Jakaya Kikwete

Naye Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya leo.

"Ndugu na marafiki nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha Bibi yetu Bi. Nuru Khalfan Kikwete kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana" Amesema Ridhiwan Kikwete.
 
Ndugu wapendwa, nawashukuru sana kwa salamu za pole na upendo kufuatia kifo cha Mama yangu mdogo mpendwa Bi Nuru binti Halfani Shomvi. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017



Advertisement
Previous
Next Post »