BAADHI YA MITAA KATA YA PANGANI YAFUATA HUDUMA ZA AFYA KM 34 - Rhevan Media

BAADHI YA MITAA KATA YA PANGANI YAFUATA HUDUMA ZA AFYA KM 34

KOKA

WAKAZI wa mtaa wa Kidimu,Miwale na Mkombozi kata ya Pangani,Mji wa Kibaha,mkoani Pwani,wanakabiliwa na adha ya kutembea umbali wa km 34 ama kutumia usafiri wa pikipiki kwenda na kurudi kufuata huduma za kiafya.
Aidha wakazi wa mtaa wa Lumumba katika kata hiyo,wanatembea umbali wa km 24 ,kwenda kufuata huduma za afya hali inayosababisha kupata usumbufu mkubwa.
Diwani wa kata ya Pangani,Agustino Mdachi ,aliyasema hayo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha,Silvestry Koka aliyoifanya kwenye kata hiyo.
Alisema tatizo la ukosefu wa zahanati inasababisha kuwaletea wananchi adha ya kutembea kwa wale wasio na uwezo wa kifedha na wengine kutumia sh.12 kwenda na kurudi kituo cha afya mkoani Mailmoja na hospitali ya rufaa ya Tumbi.
“Tunafanya jitihada za kujenga zahanati katika mtaa wa Kidimu itakayorahisisha kusogeza huduma za afya kwa wakazi wa mitaa hiyo kuliko kwenda mbali”alisema.
Mdachi alieleza kwamba,kwasasa kutokana na kuona umuhimu wa huduma ya afya,wamechukua hatua za kuamua kutumia jengo la ofisi za serikali za mtaa wa Kidimu ,lililokuwa limeanza kujengwa tangu mwaka 2009 kwa nguvu za wananchi na kuligeuza kuwa zahanati.
Alisema zahanati hiyo itanufaisha mitaa minne ya Lumumba,Mkombozi,Miwale na Kidimu na itagharimu mil.39 hadi kukamilika kwake.
Diwani huyo alibainisha ,wananchi wamegharimu sh.mil.23,halmashauri kupitia mfuko wa jimbo sh.mil 5 jumla mil.28 lakini bado wanahitaji milioni kumi.
Nae mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha,Silvestry Koka,alisema huduma za afya ni muhumi katika jamii kwa kutambua hilo,amechangia milioni tano .
Alisema ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo kutatua kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo za kielimu,afya,miundombinu na kuwezesha vijana na wanawake .
Hata hivyo mganga wa zahanati hiyo ya Kidimu,dk.Tuli alisema jengo la zahanati limefika hatua nzuri ya kukamilika.
Alisema licha ya kuwa kwenye hatua ya kuridhisha ili liweze kuanza kazi lakini kunatakiwa kujengwa jengo la uzazi litakalohudumia akinamama na watoto.
Previous
Next Post »