Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete jana amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu.
Taasisi hiyo inajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umaskini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabia nchi. Baada ya uzinduzi huo Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Rais huyo mstaafu kupitia akaunti yake ya Facebook:
“Hongera Sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzindua Mfuko Wa Wakf Wa Jakaya Kikwete Foundation. Natumai utaitumikia vema nchi yetu na bara la Afrika katika ustaafu wako. Jambo moja kubwa uwekeze kwalo ni kuandaa Viongozi Vijana. Naona timu imesheheni watu wenye uwezo mkubwa. Kila la kheri
Sign up here with your email