WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWAPIGA MSASA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA ARDHI - Rhevan Media

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWAPIGA MSASA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA ARDHI

1

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)  David Kanyatta akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii  kuhusu madhara ya kulishia  mifugo  ndani ya  hifadhi kunavyoathiri  sekta ya utalii katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma .2
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein,   akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka  Wizara ya Maliasili na Utalii  kuhusu utalii wa baharini ambao umekuwa haupewi kipaumbele katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa katika semina hiyo.33
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha, (katikati) akichangia hoja mara baada ya mada kuweza  kuwasilishwa na wataalamu kutoka  Wizara ya Maliasili na Utalii  kuhusu wanyamapori waharibifu wa mazao kama vile tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura wake kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo .4
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge  ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye, (katikati)    Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani  ( wa kwanza kulia)  wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe wa kamati hiyo wakati walipokuwa wkichangia hoja  kuhusu mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka  Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi,  tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini, iliyofanyika jana mjini Dodoma.5
Mjumbe wa  Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB ( wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na  wataalamu wa Wizara hiyo   kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi,  tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande wa kushoto ni viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii .6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia)  pamoja na  na viongozi wa taasisi katika  semina   ya kamati ya Bunge    Ardhi, Maliasili na Utalii iliyofanyika  jana mjini Dodoma .
Previous
Next Post »