WAKUU WA SHULE ZA DAR AMBAZO ZIMESHIKA MKIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE WATUMBULIWA - Rhevan Media

WAKUU WA SHULE ZA DAR AMBAZO ZIMESHIKA MKIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE WATUMBULIWA

Tokeo la picha la SHULE SECONDALI DAR KITONGA

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne  kwama 2016 yametoka na miongoni mwa Shule 10 zenye Wanafunzi waliofeli zaidi Tanzania, 6 zinatoka Dar es salaam na hiyo imemfanya Mkuu wa wilaya ya kigamboni Hashim Mgandilwa kufanya uchunguzi kwenye hizo shule.

Baada ya uchunguzi wake Mkuu huyu wa wilaya ameagiza kushushwa vyeo kwa Wakuu wa shule mbili za za Sekondari ambazo ni Kidete na Somangila Day na ametoa sababu mbili za kuchukua uamuzi huo.

Amesema sababu ya kwanza ni kufelisha na pili kuna mmoja amepata ukuu wa shule katika namna ambayo ina ukakasi na inaonekana kwa namna moja ama nyingine kuna Watu walimtengenezea kukipata hicho cheo

"Hiyo ilileta mvutano shuleni na baadhi ya Walimu walimuunga mkono na wengine hawakumuunga mkono hivyo ikasababisha Walimu takribani 7 kuihama shule hiyo kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu." Amesema  DC Mgandilwa

Previous
Next Post »