URUSI YAWAKAMATA WATAALAMU 3 WA MITANDAO IKIWALAUMU KWA USALITI NCHI - Rhevan Media

URUSI YAWAKAMATA WATAALAMU 3 WA MITANDAO IKIWALAUMU KWA USALITI NCHI

Makao makuu ya ulinzi nchini UrusiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMakao makuu ya ulinzi nchini Urusi
Wataalamu watatu wa ulinzi wa mtandano wamefunguliwa mashtaka ya uhaini nchini Urusi kwa kusaliti taifa lao kwa Marekani.
Wakili wa mmoja wa washukiwa hao, amesema watatu hao ni pamoja na mkurugenzi mkuu wa kituo cha kitaifa cha ulinzi wa habari, Sergei Mikhailov, mfanyakazi mwingine wa shirika hilo Dmitry Dokuchayev na mfanyakazi wa mahabara ya Kapspersky Ruslan Stoyanov.
Hakuna habari yoyote kuhusu kile kilichosababisha kukamatwa kwao, lakini kuna fununu kuwa huenda inahusiana na habari za idara ya ujasusi nchini Marekani kuwa urusi iludukua mtandao wakati wa CIA: uchaguzi wa urais nchini Marekani.
FSB HQHaki miliki ya pichaEPA
Image captionOne of the arrested men was the FSB's deputy head of cyber-security
Lakini msemaji wa Rais Vladimir puttin, Dmitry Peskoc amesema kukamatwa kwao hakuhusiani na madai hayo ya udukuzi ambayo Urusii imekana.
Madai mengine yanasema kuwa watatu hao walikuwa na uhusiano la kundi la kudukua mitandao linalojulikana kama Shaltai Boltai, ambalo ni maarufu kwa kutafuta mambo machafu kutoka kwa wanasiasa nchini Urusi na kuyaweka hadharani.
Previous
Next Post »