Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa amemuonya rais wa Marekani Donald Trump, dhidi ya kuachana na suala la uwepo wa mataifa mawili kwenye mzozo kati ya Israel na Palestina, akisema kuwa hakuna njia mbadala.
Hii inajiri baada ya Trump kuenda kinyume na sera za Marekani za miongo kadha, akisema kuwa ataunga mkono njia yoyote ili ambayo itachangia kuwepo kwa amani.
Wapalestina walighadhabishwa dalili kuwa kuwa kuna uwezekano kuwa hjuenda Marekani ikaacha kuunga mkono uwepo wa taifa la Wapalestina.
Mazungumzo ya mwisho ya amani kati wa Israel na Palestina yalivunjika mwaka 2014.
Akizungumza alipokutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumatano, Rais Trump aliahidi kuleta makubaliano makubwa ya amani.
Uwepo wa mataifa mawili kwa mzozo huo wa miongo kadha kati ya Isreal na wapalestina, ndilo lengo la viongozi wao na jamii ya kimataifa.
Serikali ya Israel ina matumaini ya kuwepo uhusiano mwema na Marekani baada ya miaka minane ya tofauti na utawala wa zamani wa Rais Obama.
Mkutano kati ya Israel na Marekani ndio wa kwanza wa ana kwa ana tangu Trump apate ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Lakini Ufaransa ambayo mwezi Januari iliandaa mkutano wa kuunga mkono uwepo wa mataifa mawili, ilionekana kutofurahishwa na mabadiliko hayo ya ghafla .
Sign up here with your email