Tunapenda kuwataarifu wananchi kwamba kwa mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni wanne (4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa msichana anayetuhumiwa kusababisha tukio hilo.
Hivyo Mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake.
Hakuna Wanajeshi waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, kambi za Jeshi wanaishi Wanajeshi pamoja na familia zao hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na Wanajeshi mkoani Tanga ni kuupotosha umma.
Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira potofu kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
==> Tazama video hapo chini kama tukio hilo lilikupita
Sign up here with your email