TAARIFA KWA UUMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA - Rhevan Media

TAARIFA KWA UUMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

BANG1

KWAMBA TAREHE 1.02.2017 MAJIRA YA SAA   15:45HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE – SOKONI KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA SAMWEL HOSEA MIAKA 24, MKAZI WA KIJIJI CHA KABANGAJA, AKIWA NA NOTI BANDIA 25 ZA SHILINGI ELFU KUMI KILA MOJA ZENYE JUMLA YA THAMANI YA TSH 250,000/=.
AIDHA ASKARI WALIENDELEA NA DORIA NA MISAKO NA ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 20:30HRS USIKU YA TAREHE TAJWA HAPO JUU KATIKA ENEO LA NYAMANORO ILIYOPO WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWNZA, ASKARI WALIFANIKIWA KUMKAMATA KIJANA MWINGINE WA KIUME ALIYEJULIKANA KWA JINA LA PAUL FAIDA MIAKA 21, MKAZI WA GEITA AKIWA NA NOTI BANDIA 12, ZA SHILINGI ELFU KUMI ZIKIWA NA JUMLA YA THAMANI YA TSH 120,000/=, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI ASKARI WAKIWA KWENYE  DORIA NA MISAKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO YA IGOMBE – SOKONI NA NYAMARO WAPO WATU  AMBAO INASEMEKANA WANAMILIKI NOTI BANDIA, POLISI  WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA KATIKA MAENEO HAYO, AMBAPO MISAKO NA UPELELEZI ILIFANYIKA KATIKA MAENEO YOTE KWA PAMOJA  NA KUFANIKIWA KUWATIA NGUVUNI WAHALIFU HAO.
WATUHUMIWA WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, ASKARI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUBAINI MAHALI AMBAPO NOTI HIZO ZA BANDIA ZINATENGENEZWA NA WATU WENGINE  AMBAO WANAOSHIRIKIANA NA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU KATIKA KUFANIKISHA UHALIFU.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA  ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI KUWEZA KUENDELEA KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WA MWANZA, LAKINI PIA ANAWATAKA VIJANA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA UHALIFU ILI WASIJE WAKAINGIA KWENYE MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA PILI,
KWAMBA TAREHE 01.02.2017 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI ULIPO KIJIJI CHA ILYAMCHELE TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA PAMOJA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WA SERIKALI YA BUHINDI WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA EKARI MBILI NA NUSU AMBALO LILIKUWA NDANI YA HIFADHI HIYO.
POLISI WALIPOKEA TAARIFA ZA UWEPO WA SHAMBA HILO LA BHANGI KUTOKA KWA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU HUO, NA KWAMBA WANANCHI AMBAO WANAOISHI KARIBU NA MSITU NDIO WALIOPANDA BHANGI HIYO KATIKA ENEO HILO NA PINDI WANAPOKATAZWA WAACHE TABIA HIYO WAMEKUWA WAKIKAIDI NA KUWATISHIA KUWAPIGA KWA MAWE MAAFISA WA HIFADHI HIYO. ASKARI WALIKWENDA PAMOJA NA MAAFISA HAO HADI ENEO LA HIFADHI YA MSITU NA KUKUTA ENEO LA EKARI MBILI NA NUSU LIKIWA LIMEOTESHWA BHANGI, ASKARI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA HILO LA BHANGI LILILOKUWA NA JUMLA YA IDADI YA MICHE 7300 YA BHANGI. POLISI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUWABAINI WATU AMBAO WALIHUSIKA NA KUOTESHA BHANGI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI.
AIDHA KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE 02.02.2017 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KAFUNZO KILICHOPO WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA,   ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA MKORO MSAMI MIAKA 74, MKAZI WA KIJIJI CHA MAFUNZO, KWA KOSA LA KUOTESHA MICHE 84 YA BHANGI KWENYE SHAMBA LENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA MTU KATIKA KIJIJI TAJWA HAPO JUU ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI JUU YA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA PAMOJA NA SHAMBA LAKE NA KUANZA ZOEZI LA  KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI KATIKA SHAMBA HILO KISHA KUITEKETEZA KWA MOTO.
MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA ASKARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIAKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA  NA MISAKO KATIKA MAENEO YOTE ILI KUWEZA KUWAKAMATA NA KUWADHIBITI WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI, ILI LIWEZE KUWAKAMATA NA KUDHIBITI WATU WOTE AMBAO WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA,
ACP: AUGUSTINO SENGA
KAIMU KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Previous
Next Post »