Utawala nchini Nigeria unawatafuta maafisa wawili wa vyeo vya juu katika idara ya forodha wanaokisiwa kuhusika katika kuingiza nchini humo silaha.
Silaha hizo zinaripotiwa kupatikana ndani ya lori moja kwenye bandari ya mji wa Lagos siku ya Jumatatu.
Maafisa wa idara ya forodha waliwakamata watu watatu wakati lori hilo lilinaswa.
Hameed Ibrahim Ali, afisa mkuu wa idara ya forodha anasema masanduku 49 yakiwa na bunduki 661 yalinaswa.
Alisema kuwa aina ya bunduki zilizonaswa ni haramu nchini Nigeria.
Sign up here with your email