Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy ameagizwa kuunda tume ya kuchunguza tukio la kuungua kwa bweni la wasichana liitwalo Serengeti la Itamba sekondari mkoani Ruvuma, pamoja na bweni lingine la wasichana lililoungua Jumamosi iliyopita.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipotembelea shule hiyo kujionea athari za moto huo ulioteketeza bweni moja lote
Amesema serikali haiwezi kukubali na ni lazima chanzo cha moto huo kijulikane na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika endapo uchunguzi utabainisha kuwa kuna watu wamehusika.
Mhe. Olesendeka amesema serikali haiwezi kukubali vitendo vya moto kuendelea kuunguza shule mbali mbali hapa nchini.
Pia ameuagiza uongozi wa shule hiyo kuweka Mazingira mazuri kubaini ukweli wa hujuma kama hizi zinazoweza kujitokeza lakini pia kama kuna dosari mbali mbali miongoni mwa wanafunzi au shule nzima zijulikane ili ufumbuzi upatikane.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka(wapili kushoto) akiangalia athari za moto wa bweni hilo
Mabaki ya vitu vya wanafunzi vilivyoteketea kwa moto katika bweni hilo
Mkuu wa mkoa akizungumza na wanafunzi shuleni hapo
Sign up here with your email