MANISPAA YABANWA MATUMIZI YA FEDHA ZA VIJANA - Rhevan Media

MANISPAA YABANWA MATUMIZI YA FEDHA ZA VIJANA

Madiwani Manispaa ya Morogoro

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wameitaka kuwekwa wazi kwa asilimia 5 ya mapato ya halmashauri hiyo ambayo yanapaswa kutolewa kama mikopo kwa vijana na wanawake,
 Hatua hiyo inakuja kufuatia malalamiko ya wananchi wengi kuwa hawajui fedha hizo zimekuwa zikitumiwaje na halmashauri hiyo huku madiwani nao wakishindwa kuwa na majibu ya kuridhisha juu ya suala hilo.
Doroth Mwamsiku, diwani wa viti maalum akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo amesema, taarifa za mikopo hiyo kwa wanawake na vijana zinapaswa kuwa wazi ili wananchi waweze kunufaika na fedha hizo.
“Taarifa hizo zinatakiwa kuwa wazi kwa kila kata ili ijulikane ni vikundi gani vinapata fedha hizo sambamba na kuwepo kwa taarifa za mrejesho wa mikopo hiyo.
“Tunapofika kwenye mikutano na wananchi tunakumbana na maswali mengi, likifika hilo la mikopo ya makundi hayo ndipo sisi madiwani tunapokosa majibu ya kutosha,” amesema.
Akijibu hoja hiyo Pascal Kihanga, Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo amewataka madiwani kujenga mahusiano ya karibu na viongozi wa kata ili waweze kupata taarifa hizo.
“Taarifa za matumizi ya fedha hizo zipo, kinachotakiwa ni nyie kuwa na mahusiano mazuri na watendaji wa kata ambayo yatawafanya mpate majibu sahihi mnapofika kwenye mikutano na wananchi,” amesema Kihanga.
Previous
Next Post »