Waziri
wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiwa
ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa tatu
kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics,
Jack Feng (kushoto) wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo
ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae
"Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. Waziri
Mwijage ameridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho na
kumpongeza muwekezaji wake hasa kwa kasi wanayoenda nayo. Kwa mujimu wa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics ambao ndio
wamiliki wa kiwanda hicho, amesema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwezi
septemba mwaka huu, kiwanda hicho kitakuwa kimekamilika na kitaanza
kufanya kazi. Uwepo wa kiwanda hicho, utaweza kufungua fursa za ajira
kwa vijana mbalimbali nchini.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (katikati) akizungumza jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng
(kulia) wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha
kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze
Mkoani Pwani.
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia) akimuonyesha kitu,
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage wakati walipokuwa
wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo
litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo
katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akimsikiliza Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe wakati akimueleza jambo, wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.
Sign up here with your email