WAKAZI WA CHAGA A NA B HUKO KILOMO WATESEKA KWA KUKOSA MAJI SALAMA - Rhevan Media

WAKAZI WA CHAGA A NA B HUKO KILOMO WATESEKA KWA KUKOSA MAJI SALAMA

KAAWA

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wakazi wa kata ya Kilomo na kusikiliza kero zinazowakabili. (picha na Mwamvua Mwinyi)

WAKAZI wa kijiji cha Chaga A na B ,kata ya Kilomo,wanateseka kwa kukosa huduma ya maji safi na salama huku wakiitupia lawama DAWASCO Bagamoyo ambayo wamedai inashindwa kuwatatulia adha hiyo.
Wamesema tangu vijiji hivyo viwe vichanga miaka ya 1985 ,hawajapatiwa ufumbuzi juu ya kero hiyo na imebaki kuwa hadithi.
Aidha vijiji hivyo vinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme hivyo wamemuomba mbunge wa jimbo hilo.dk.Shukuru Kawambwa awasaidie.
Hayo yalijiri, wakati dk.Kawambwa alipokwenda kwenye ziara yake kata ya kilomo .
Baadhi ya wakazi hao akiwemo Charles Petro na Mngindo,waliiomba serikali na mbunge huyo kuwatatulia changamoto hizo.
Walisema awali walikuwa wakitumia visima vya asili lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa wanategemea maji ya bomba ya kununua kwenye viosk .
Petro alisema ,licha ya tegemeo hilo maji yamekuwa yakikatika mwezi mzima hivyo kushindwa kuoga na kuweka mazingira safi majumbani.
“Dawasco inazembea ,sisi tunashida ya maji,tangu Chaga A haijawa kijiji miaka ya 1985, wakazi  30 ambapo sasa wapo 3,500 ,lakini miundombinu ya maji hakuna”.
Kuhusu EPZ walisema wanunuzi wanakatishwa tamaa kuwa hakuna maeneo ya kununua wakati wapo waliopisha eneo hilo na wengine wahahusiani na jambo hilo.
Akijibu kuhusiana na changamoto hizo,Dk Kawambwa alieleza kwamba,chanzo cha Ruvu chini kinatumiwa na maeneo mengi ya wilaya hiyo lakini tatizo kubwa ilikuwa maji hayatoshi kutokana na idadi ya watu kuongezeka  na kulisha Kibaha na Dar es salaam.
Alisema kwasasa mabomba makuu ya usafirishaji yameshalazwa na mtandao wa mabomba ukiendelea kutandazwa ili mradi huo ukimalizika uweze kuondoa adha ya maji.
Dk.Kawambwa alisema ,ataendelea kufuatilia tatizo hilo,kwa kuzungumza na kushirikiana na dawasco kujua hatua zinazoendelea na kubadilishana mawazo pale itakapobidi.
Kuhusu nishati ya umeme alisema changamoto hiyo itakuwa historia baada ya vitongoji vyote vya kata ya Kilomo kuingizwa katika awamu ya tatu ya REA .
“Awamu ya kwanza na ya pili nilikosa lakini kwa sasa vitongoji vingi vimeingizwa katika mpango wa umeme vijijini ikiwemo Changa A na B .
Kuhusiana na EPZ alisema,mwaka 2012/2013 bunge iliidhinisha kiasi cha sh.bil.52 kwa ajili ya kulipa fidia za watu waliopisha eneo hilo hivyo  tatizo lingekuwa limeisha zamani.
Mbunge huyo alisema ,atahsirikiana na diwani wa kata ya Kilomo kufuatilia suala hilo kwa kina  ili kujua mchakato umekwama wapi.
Dk.Kwambwa amemaliza ziara yake ya kutembelea kata 11 zilizopo jimboni hapo ambapo amechukua kero zote alizofikishiwa na kuahidi kuzifuatilia panapo husika.
Previous
Next Post »