WAHESHIMIWA WABUNGE WA KAMATI YA MALIASILI, ARDHI NA UTALII, LEO WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA PAMOJA NA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO- KIJITONYAMA JIJINI DAR ES SALAAM KUJIONEA URITHI WA TAIFA TULIONAO. - Rhevan Media

WAHESHIMIWA WABUNGE WA KAMATI YA MALIASILI, ARDHI NA UTALII, LEO WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA PAMOJA NA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO- KIJITONYAMA JIJINI DAR ES SALAAM KUJIONEA URITHI WA TAIFA TULIONAO.

SUSHA

Mwenyekiti wa  Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii  wakati walipokuwa wakiangalia sanamu mtu wa kabila la Kimasai iliyochongwa kwa kutumia mti aina ya Mpingo kabla ya Wabunge wa kamati hiyo kuanza kutembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Eng. Ramo makani.SUSHA 1
 Mwenyekiti wa  Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye ( watatu kushoto)   na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng.Ramo Makani (watatu kulia)  akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi  (wa pili  kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi  wa Wizara ya Maliasili na Utalii  wakati walipokuwa wakiangalia zana za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale wakati  Wabunge wa kamati  ya Maliasili, Ardhi na Utalii walipokuwa wakitembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.SUSHA 2
Mwenyekiti wa  Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akitia saini kwenye kitabu cha Wageni  akishuhudiwa na baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii   pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii  wakiwa kwenye chumba maalumu ( strong room)  cha kuhifadhia urithi wa utamaduni wa thamani kubwa kama zamadamu (hominine remains), masalia ya akiolojia, historia pamoja na sanaa ya ethnografia) leo   walipotembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam, SUSHA 3
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Eng. Ramo makani (kushoto) akitia msisitizo jambo kwa Mwenyekiti wa  Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (katikati) akiwa  pamoja na Mbunge wa kamati hiyo, Mhe, Shabani Shekilindi ( wa kwanza kulia) mara baada ya kumaliza ziara ya  kutembelea kijiji cha  Makumbusho cha Kijitonyama, jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akiwaelezea Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii  kuhusu meli ya kivita ya iliyozama baharini iliyotumiwa na jeshi la Kijerumani wakati wa vita vya kwanza duniani (1914-1919)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili,  Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye wakati wakielekea kuangalia Nyumba ya wahehe iliyopo kijiji cha  Makumbusho cha Kijitonyama, jijini Dar es Salaam,  ( Picha na Lusungu Helela- WMU)
Previous
Next Post »