TOFAUTI KATI YA UKUTA WA TRUMP NA KUTA ZINGINE MAARUFU ZILIZOJENGWA - Rhevan Media

TOFAUTI KATI YA UKUTA WA TRUMP NA KUTA ZINGINE MAARUFU ZILIZOJENGWA


Image captionMpaka kati ya Mexico na Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuendelea na mipango yake ya kujenga ukuta wa urefu wa kilomita 3000 kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico.
Ukuta huo utakuwa na urefu wa kati ya mita 9 na 16 na utajengwa kwa kutumia changarawe.
Warepublican na wafuasi wao wanasema kuwa ukuta huo utawazui raia wa Mexico wanaoingia Marekani kinyume na sheria.
Tayari kuna ua kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani.

Sehemu moja kwenye ua kati ya Marekani na Mexico walinzi uruhusu watu kuongea na marafiki zao na jamaaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSehemu moja kwenye ua kati ya Marekani na Mexico walinzi uruhusu watu kuongea na marafiki zao na jamaa

Kuna kuta nyingi katika historia ambazo zilijengwa na kutenganisha mataifa. Lakini zinafananishwa vipi na mpango wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Ni miaka 27 iliyopita tangu ukuta wa Berlin kubomolewa.

Tutaanza na ukuta wa Berlin:
Kwa hili tutaangazia nyuma miaka ya 1950 wakati Ujerumani iligawanyika pande mbili, Mashariki na Magharibi.

Ujerumani Magharini na Mashariki zilitenganishwa na ukuta wa BerlinHaki miliki ya pichaBBC NEWSROUND
Image captionUjerumani Magharini na Mashariki zilitenganishwa na ukuta wa Berlin

Wakaazi wa upande uliodhibitiwa na Ufaransa, Uingereza na Marekani wa Magharibi, waliamka siku moja mwezi Agosti mwaka 1961, na kupata ukuta kati yao na eneo lililokuwa likidhibitiwa na muungano wa kisovieti.
Mwanzo ulikuwa ni ua tu lakini baadaye ulijazwa na changarawe yenye urefi wa mita 3.6 sehemu zingine.
Ukuta wa Berlin
Ulikuwa na umbali wa kilomita 100 na ua wa kilomita 66.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUkuta wa Berlin

Ukuta wa Trump utakuwa na umbali mkubwa lakini si katika historia.

Mpaka kati ya Mareknia na Mexico una umbali wa kilomita 3000
Kwa hivyo ikiwa Trump atauzungusha sehemu kama za milima, atakuwa na changamoto za kuufana mrefu zaid kuliko ukuta wa China.

Ukuta mrefu zaidi
Image captionUkuta mrefu zaidi

Umbali kamili wa ukuta wa China haujulikani lakini inaaminiwa kuwa wakati mmoja ulikuwa na umbali wa kilomita 20,000.
Una urefu wa hadi mita saba sehemu zingine

Ukuta wa ChinaHaki miliki ya pichaTHINKSTOCK
Image captionUkuta wa China

Lakini ukuta wa Trump unaweza kushinda kuta zingine kwa urefu.

Trump hawezi kuamua ukuta huo unaweza kuwa na urefu wa kiasi gani, lakini ameshatamka urefu wa mita 16. Huo utakuwa urefu wa zaidi ya basi tatu.

Ukuta mrefu zaidi
Image captionUkuta mrefu zaidi

Ukuta wa Hadrian ambao ulijengwa kwa amri ya Emperor Hadrian mwaka wa 122AD, ulikuwa na urefu wa basi.
Ulikuwa na umbali wa kilomita 117 na ulikuwa ukitenganisha England na Scotland.

Ukuta wa HadrianHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUkuta wa Hadrian

Mada zinazohusiana

Previous
Next Post »