SIMBA USIYEMPENDA KAJA - Rhevan Media

SIMBA USIYEMPENDA KAJA


Dar es Salaam. Mabao mawili ya mshambuliaji aliyetokea benchi, Obrey Chirwa yameiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa Mwadui 2-0 jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 46, moja zaidi ya Simba iliyoporomoka katika nafasi ya pili kwa mara ya kwanza tangu Oktoba mwaka jana.
Chirwa aliyeingia akitokea benchi katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima aliifungia Yanga bao la kwanza dakika 67, akimalizia mpira uliomtoka kipa Shabaan Kado alipojaribu kuzuia shuti la Simon Msuva.
Akicheza mechi yake ya kwanza mwaka huu, Chirwa alifunga bao la pili dakika ya 80, akipokea pasi ya kichwa ya Thaban
Kamusoko kabla ya kuwadanganya mabeki kuwa angepiga na mguu wa kulia, lakini alibadilika na kutumia wa kushoto.
Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema ushindi huo umekuja kwenye wakati muhimu kutokana na uhitaji wa pointi tatu waliokuwa nao.

Previous
Next Post »