SHULE ZA DAR ZASHIKA MKIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE - Rhevan Media

SHULE ZA DAR ZASHIKA MKIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Tokeo la picha la SHULE ZA SEKONDARI DAR

Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es Salaam umeshika mkia katika shule kumi za mwisho kwenye matokeo ya kidato cha nne kitaifa yaliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam.
Katika shule 10 za mwisho kitaifa Dar es Salaam imeingiza shule sita ambazo ni Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Somangila Day na Kidete. Shule nyingine ni Masaki iliyoko mkoani Pwani, Dahani iliyoko mkoani Kilimanjaro, Ruponda mkoani Lindi na Makiba mkoani Arusha.
Matokeo hayo yametangazwa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani(Necta), Dk Charles Msonde.

Previous
Next Post »