SERIKALI YATAKIWA KUJIPANGA KATIKA UJIO WA VIWANDA –TPSF - Rhevan Media

SERIKALI YATAKIWA KUJIPANGA KATIKA UJIO WA VIWANDA –TPSF




MFUKO wa Sekta Binafsi nchini (TPSF) umesema ujio wa viwanda 200 kutoka nchini China,Serikali inatakiwa kujipanga kupokea viwanda hivyo kwani vitachangia kukua kwa uchumi pamoja na ajira nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema China kwa sasa ni nchi yenye mitaji mikubwa kuliko nyingine duniani hivyo lazima kuongeza mahusiano zaidi ili kuweza kunemeeka  nao katika kuelekea uchumi wa kati wa viwanda kufikia 2025.
Simbeye amesema viwanda vingi vya China vimefikia hatua ya kuweza kuhamishwa katika sehemu mbalimbali katika Bara la Afrika na kuendelea na uzalishaji kutokana na uhakika wa rasilimali watu pamoja na malighafi.

Amesema  kutokana na uwekezaji wa viwanda hivyo suala la maeneo tengefu  liangaliwe kimkakati   katika kufanya maandalizi  ya viwanda hivyo pamoja na vingine vitakavyojengwa.Simbeye amesema nchi ya China ina uwezo mkubwa wa mitaji kuliko maeneo mengine duniani na Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda  zilizowawezesha  kufanya mapinduzi ya viwanda.
Aidha amesema ujio wa Waziri wa Mambo ya Nchi wa China nchini  ni sehemu ya kuchangamkia fursa kwa karibu kwa kuongeza uhusiano uzidi kudumu ambao wenye maendeleo baina ya nchi mbili.

.Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi habari juu ujio wa viwanda 200 vya China kuhamishiwa Nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uwekezaji na  Maendeleo  ya Biashara wa TPSF, Edward Furaha akizungumza na waandishi habari juu ujio wa viwanda iliyofanyika  jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.