SEMINA YA MAFUNZO YA KARATE KIMATAIFA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA - Rhevan Media

SEMINA YA MAFUNZO YA KARATE KIMATAIFA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA


Mafunzo ya karate ya kimataifa yanayoambatana na kufanya mtihani wa kupanda madaraja yamefanyika Jijini Arusha yakiongozwa na Master Shihan Shalom Avitan, kutoka nchini Israel .

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Afisa michezo mkoa wa Arusha Mwamvita Okeng’o ambapo amesema kuwa serikali imeipa michezo kipaumbele ili kupunguza tatizo la ajira nchini na amewataka wanamichezo hao kuuambikiza katika jamii kwa ujumla

Akijibu risala iliyoandaliwa na West coast Shotokan internation Karate( ASS'N) Afisa michezo huyo wa mkoa amesema kuwa serikali inafanya jitihada ili kuwapatia eneo la kudumu la kufanyia mazowezi kama walivyoomba.

Naye afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno amesema kuwa michezo inaimarisha afya ,ni ajira hivyo ameitaka jamii kushiriki kikamilifu huku akiwasisitiza vijana kutumia fursa hiyo ili waweze kujiajiri.

Muandaaji wa mafunzo hayo hapa nchini Sensei Dady Ramadhan ambaye ni Mkufunzi kiongozi amesema kuwa wapo wanakarate wanaocheza Shotokan ambao wana daraja mbalimbali katika taaluma hiyo miongoni mwao wapo waliofanya mtihani na wamepanda daraja

Aidha amesema kila mwaka wanamuita mwalimu na kufanya mitihani ,hivyo amewataka wale wote wanaotaka kuifunza mchezo huo wahakikishe wanajicfunza kupitia wataalamu ambao wamepitia mafunzo hayo na wenye uzoefu wa kutosha.

“Unajua kwa sasa mchezo huu unawaalimu wengi ambao wamevamia hawana taaluma kabisa hivyo msikubali kuburuzwa na kufundishwa na hao watawapotosha na kuleta madhara kwani hawazifahamu kanuni na miiko ya karate.”alisema sensei Dady.

Wakufunzi wanaoingia kufanya mtihani wa kupandishwa madaraja wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza maelekeo kabla ya kuanza kufanya mtihani huo.

Wakwanza kushoto ni Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree ambaye ni raisi wa shirikisho la West Shotokan Karate Internation duniani ,akifuatiwa na Mkufunzi wa West shotokan Karate Kanda ya kaskazini Dady K.Ramadhan.
Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan akiwa anawapa maelekezo wakufunzi wanaofanya mtihani wa kupanda madaraja kabla ya darasa kuaza rasmi .
Wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja na Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree baada ya kumaliza kufanya mitihani kwa vitendo katika hatua mbalimbali .


Previous
Next Post »