RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWTE MGENI RASMI MIAKA 10 YA GOLF LUGALO - Rhevan Media

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWTE MGENI RASMI MIAKA 10 YA GOLF LUGALO

BRIG

Mwenyekiti wa Klabu ya  Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo wakati akizungumza na Waandishi wa habari Klabuni Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………….

 
Rais Mstaafu DR. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mashindano ya kuadhimisha Miaka 10 ya Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi ya Lugalo.
 
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya  Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo wakati akizungumza na Waandishi wa habari Klabuni Jijini Dar es Salaam.
 
Aliongeza kuwa Rais wa Awamu ya Nne yeye ndio aliezindua uwanja huu, hivyo ni fursa nzuri kujionea maendeleo yaliyofikwa katika kipindi cha Miaka 10.
 
“Uongozi umeona ni busara kumualika kama mgeni rasmi katika kutimiza miaka kumi pia ni fursa yeye kuanza kucheza na Mbali na mgeni rasmi viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wamealikwa kushiriki katika ufunguzi na ufungaji wa mashindano haya “ Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
 
Mashindano haya yatafanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Lugalo Gofu Lugalo, kuanzia tarehe 17 hadi 19 februari 2017 ambapo Wataanza wachezaji wa kulipwa (Pros) na wachezaji wasaidizi (Caddies).
 
Aliongeza kuwa Siku ya pili ya tarehe 18 Februari, watashindanishwa wachezaji wa Ridhaa (Armatures) na siku ya tatu yani tarehe 19 Februari, watashindanishwa wachezaji waliofanya vizuri tarehe 18 februari ikifuatiwa na sherehe za ufungaji wa mashindano hayo.
 
 Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo alifafanua wakati klabu inazinduliwa ilikuwa na mashimo Tisa tu ya mchezo huu (9 Holes), lakini kwa sasa imefanikiwa kuwa na mashimo kumi na nane (18 Holes) kama mchezo huu unavyohitaji.
 
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema kutokanana na kuwa mashindano makubwa sheria za ndani zimeandaliwa ambazo hazitapingana na Sheria za Kimataifa.
 
“ Wachezaji watambue kuwa tutafuata Mwongozo wa Kimataifa wa kuendeshha mashindano ili kuwa na sifa za kimataifa na kuiletea sifa nchi katika uandaaji wa mashindano yenye viwango” alisema Kapteni Masai.
 
Kwa Upande wake Mmoja wa Wadhamini wa Michuano hiyo kutoka kampuni ya Bima ya Resolution  Kaimu Meneja wa Masoko Marcellino Mitawa  alisema wameamua kuongeza nguvu katika golf ili kuondoa dhana kuwa ni mchezo wa matajiri.
Previous
Next Post »