PICHA: RAIS MAGUFULI AKIZINDUA MRADI WA MABASI YA MWENDO WA HARAKA - Rhevan Media

PICHA: RAIS MAGUFULI AKIZINDUA MRADI WA MABASI YA MWENDO WA HARAKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 25, 2017 amefungua miundombinu na utoaji wa huduma ya mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kabla ya ufunguzi wa huduma hiyo, Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania hasa waishio karibu na barabara za mwendokasi kutunza miundombinu yake.
Aidha, amesema serikali yake imetenga bilioni 38 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za ndani zilizoko katika jiji la Dar es Salaam, kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari pamoja na kulifanya jiji hilo kuwa la kisasa hususan kwamba linakua kwa kasi.
“DSM ni jiji la biashara, na ni miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi barani Afrika, hivi sasa lina wakazi milioni tano na kwamba hapo baadae linataraji kuwa na wakazi milioni 10,” amesema.
Rais Magufuli amesema awali nchi ilikua inapoteza fedha kiasi cha bilioni 411.5 kwa mwaka, huku Dar es Salaam iliongoza kwa kupoteza bilioni 4 kwa siku kwa sababu ya changamoto ya foleni na kwamba, awamu za ujenzi wa mradi huu ambazo ni sita zikikamilika zitachochea ongezeko la mapato pamoja na kuboresha hali ya kiuchumi kwa wananchi.
Naye Makamu wa Rais Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika ambayo imefadhili ujenzi wa mradi huo awamu ya kwanza kwa zaidi ya bilioni 400, Makhtar Diop, amesema benki yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa serikali hasa katika miradi ya ujenzi wa miundombinu.
“Tunaipongeza serikali yako kwa kujenga mfumo wa usafirishaji wa haraka, hata nchi yangu ya Senegal itaanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi ya haraka sababu husaidia watu kusafiri haraka, unaimarisha mahusiano mazuri kazini na katika familia sababu watu hawatachelewa tena kwenda kazini ama kurudi nyumbani,”amesema.
Diop amemhakikishia Rais Magufuli kuwa benki yake itafadhili mradi wa ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo (Ubungo Fly Over).
“Tunaona matokeo mazuri ya mradi wa BRT, umeboresha makazi ya watu, ikiwemo ujenzi wa maduka ya kisasa, benki ya dunia itaendelea kutoa ushirikiano, hivi karibuni nitaupeleka mradi wa Ubungo Fly Over katika bodi ya benki ujadiliwe ili uweze kufadhiliwa,” amesema.
Hivi sasa huduma ya mabasi yaendayo haraka, inahudumia zaidi ya abiria laki mbili kwa siku, hadi mwishoni mwa mwezi, Disemba 2016 mapato yake yaliongezeka kutoka milioni 382 kwa mwezi ulipoanza, hadi kufikia bilioni 3.9.
MO Blog imekuwekea picha jinsi uzinduzi huo ulivyofanyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza kulia wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka kadi ya Kieletroniki katika Mashine ya UDART ilikuweza kupita kama ishara ya Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene akimuelekeza jambo katika mashine hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wanahabari mara baada ya kuzindua utoaji huo wa huduma ya usafiri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuendesha gari la Mwendo Kasi katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) mara baada ya kufungua rasmi Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya Usafiri wa Haraka (BRT).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakati Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop akimtunza msani Mrisho Mpoto wakati alipokuwa akitumbuiza katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka BRT-Kariakoo huku Rais Dkt. Magufuli akifurahia. Picha na Ikulu.
Previous
Next Post »