NIPO TAYARI KUOLEWA - ASHA BOKO - Rhevan Media

NIPO TAYARI KUOLEWA - ASHA BOKO


Msanii wa maigizo ya vichekesho Asha Boko amesema ameishi katika maisha ya upweke kwa miaka 8 baada ya mume wake kufariki. 

Asha Boko
Akiongea kupitia eNewz Asha amesema aliamua kukaa peke yake baada ya mume wake kufariki na aliamua kulea watoto wake peke yake bila kuwa na baba wa kufikia kwa kuwa aliogopa usumbufu wa wanaume kwani huenda wangewanyanyasa watoto wake.
Hata hivyo Asha amesema kwa sasa akitokea mtu ambaye yupo tayari kumuoa na ambaye atakubaliana na kazi yake yupo tayari kufunga ndoa kwa kuwa yeye ni mtoto wa kiislam na dini ina ruhusu.  
Previous
Next Post »