Ndege ya jeshi la Nigeria imewaua kimakosa raia na kuwajeruhi wengine katika eneo la Rann kaskazini mashariki mwa nchi.
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, linasema kuwa takriban watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa
Wafanyakazi wa kutoa misaada ni baadhi ya wale waliouawa huku shirika la msalaba mwekundu likisema kuwa 6 kati ya wafanyakazi wake waliuawa.
Shambulizi hilo lilitokea karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon ambapo jeshi la Nigeria limekuwa likipigana na kundi la Boko Haram.
Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Lucky Irabor, anasema kwa rubani wa ndege kimakosa aliamini kuwa alikuwa akiwashambulia wapiganaji.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametuma rambi rambi akisema kuwa amehusunishwa na kupotea kwa maisha na kuomba kuwepo utulivu.
MSF inasema kuwa watu wengi waliouawa ni wale waliohama maeneo ambapo Boko Haram walikuwa wemeendesha mashambulizi.
Sign up here with your email