NEC YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR - Rhevan Media

NEC YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR



Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani leo. Kulia Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst. Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe mara baada ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani leo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo la Dimani. Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa pili ), Msimamizi Msaidizi wa jimbo la Dimani Bi. Idaya Selemani Hamza (katikati), Mkurugenzi wa huduma za kisheria, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
Orodha ya Majina ya Wapiga kura iliyobandikwa Siku nane kabla ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika kituo cha kupigia kura cha Nyamanzi chenye wapiga Kura 603 katika jimbo la Dimani leo. 


Previous
Next Post »