Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Karatu mkoani
Arusha, Thomas Darabe na wenzake saba wamepandishwa kizimbani kujibu
shitaka la kuharibu mali ya thamani ya zaidi ya sh milioni 75.4 na
vitunguu.
Pamoja
na Darabe, waliopandishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha/
Arumeru ni Charles Lameck ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia
maji ya ya vijiji saba vilivyoko katika wilaya ya Karatu na George Pius.
Wengine ni Baridi John, Christopher Lameck, Florian Tiofil, Daniel Ninida na Lazaro Emmanuel.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya watumia maji alishitakiwa na mashitaka manne pekee yake
ya thamani ya zaidi ya sh milioni 60 katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha
na Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.
Akisomewa
shitaka la kwanza na Mwendesha mashitaka wa serikali, Charles Gakirwa
mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, alidai kuwa Desemba 28 mwaka huu
mtuhumiwa alifanya uharibifu wa mali aina ya pampu ya maji ya thamani
ya sh milioni tatu na bomba la maji la sh 448,000.
Shitaka
la pili lililosomwa wakili wa serikali Gakirwa mbele ya hakimu mkazi wa
wilaya ya Arusha , Devotha Msofe ilidaiwa kuwa Lameck alifanya
uharibifu katika wa mfumo wa maji katika kijiji cha Quandet Karatu wa
thamani ya zaidi ya sh milioni 1.6.
Mtuhumiwa
alikana mashitaka yote na alipewa dhamana ya mtu mmoja na wadhamini
wakifanikiwa kukidhi vigezo vyote katika mashitaka hayo.
Katika
mashitaka yaliyowahusu washitakiwa wote, akiwemo Darabe pamoja na
Lameck ilidaiwa kuwa wote kwa pamoja walitenda kosa la uharibifu wa mali
kwa kuchoma pampu ya maji ya thamani ya zaidi ya sh milioni tatu na
injini ya maji ya thamani ya sh milioni 12.
Shitaka
la tatu lililokuwa likiwakabili washitakiwa wote ni kuharibu mazao aina
ya vitunguu ya thamani ya zaidi ya sh milioni 49 na pampu mbili za sh
milioni sita.
Washitakiwa
wote walikana mashitaka hayo na dhamana zao zilikuwa wazi na upelelezi
wa kesi hiyo ulikuwa bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena
januari 16 mwaka huu.
Sign up here with your email