Mvumbuzi mmoja wa
Ghana ameonyesha kile anachotaja kuwa uvumbuzi wake wa hivi karibuni
unaoshirikisha magari katika maonyesho ya Kiteknolojia katika mji mkuu
wa Accra.
Kwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya
Katanka na mbaye pia ni kiongozi wa dini alionyesha gari alilotengeza
aina ya V8, pikipiki za magurudumu matatu, mashine za roboti za
kuchomelea vyuma miongoni mwa vinginevyo.Alitengeza gari lake la kwanza mwaka 1998 na tangu wakati huo chapa yake ya Kantanka imetoa magari kadhaa ikiwemo magari yenye magurudumu manne na SUV.
Sign up here with your email