Mwanamume anayeshukiwa kufanya shambulizi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwenye klabu moja ya burudani mjini Istanbul, alipata mafunzo yake nchini Afghanistan, kwa mujibu wa gavana wa mji huo.
Vasip Sahim, alisema kuwa mwanamume huyo kwa jina Abdulkadir Masharipov raia wa Uzbekistan, anaaminiwa kuingia nchini Uturuki mwezi Januari mwaka 2016.
Bwana Sahi anasema kuwa mshukiwa amekiri kuendesha shambulizi hilo na alama zake za vidole zilifanana na zile zilizopatikana eneo la mkasa.
Watu 39 waliuawa wakati wa shambulizi hilo ambapo pia watu kadha walijeruhiwa.
Raia wa Israel, Ufaransa, Tunisia na Lebanon, India, Ubelgiji, Jordan na Saudi Arabia walikuwa ni baadhi ya waathiriwa.
Kundi linalojiita Islamic State linasema kuwa ndilo liliendesha shambulizi hilo, kulipiza kizazi harakati za jeshi la Uturuki nchini Syria.
Polisi walimamkamata mtu huyo siku ya Jumatatu katika vitongoji vya mji wa Istanbul.
Sign up here with your email