MRADI WA MAJI KATA ZA KIBINDU NA KWAMDUMA JIMBO LA CHALINZE WAZINDULIWA, WANANCHI WAANZA KUPATA MAJI - Rhevan Media

MRADI WA MAJI KATA ZA KIBINDU NA KWAMDUMA JIMBO LA CHALINZE WAZINDULIWA, WANANCHI WAANZA KUPATA MAJI

RI1“Maji ni Uhai” Katika kuhakikisha kuwa Maji ya Uhakika yanapatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Mheshimiwa Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwan Kikwete aliamua kufanya Ziara katika Chanzo Cha Maji Wami na miundo mbinu yake ili kuona maendeleo ya ujenzi wa awamu ya tatu ya mradi huo wa Maji,  Kazi inakwenda vizuri na ni matarajio kuwa mradi huu utakamilika mapema ili kutatua shida ya maji katika halmashauri hiyo, Mradi huu umegharimu kiasi cha fedha za kitanzania milioni 26 na tayari kata za Kibindu na Kwamduma zimeanza kupata majiRI2
Diwani wa kata ya Kibindu kwa niaba ya Mbunge akimbebesha mmoja wa Mwanakijiji kama ishara ya kufungua mradi huo
Wananchi wa kijiji cha Kwamduma sasa wanapata Maji safi baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji kijiji hapo. Mradi huu umegharimu kiasi cha fedha za kitanzania milioni 26 ambapo umeweka koki 10 za kutekea maji.RI3
Hali ilivyokuwa kijiji cha Kwamduma, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kabla ya Uzinduzi wa mradi wa Maji Jana 24 January 2017.RI4
Diwani wa kata hiyo Bwana Mkufya akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama  mkazi wa kijiji hicho  katika hafla hiyo ya uzinduzi.RI5
Diwani akishangilia kukamilika mradi huo ambao utawawezesha wananchi kuchota maji muda wote. Mradi huo umewekewa sola ili kuwezesha wananchi kuchota maji hadi wakati wa usiku.
Previous
Next Post »