Maafisa wa polisi
wamewakamata raia wawili wa Morocco ambao walijaribu kuwaingiza
wahamiaji katika eneo linalotawaliwa na Uhispania lililo kazkazini mwa
Afrika la Cueta- wawili hao wakiwa wamejificha ndani ya gari na mwengine
katika sanduku.
Wakati maafisa wa polisi walipokagua gari moja
siku ya Jumatatu ,mtu mmoja alipatikana amefichwa katika eneo la mbele
la gari na mwengine amefichwa katika eneo la kiti cha nyuma cha gari.Mwanamume huyo na mwanamke ,wanaodaiwa kuwa raia wa Guinea ,walipata huduma ya kwanza kwa kuwa walikuwa na hewa kidogo ya kupumua.
Kisa hicho kilitokea mnamo mwezi Disemba 30 na mtu huyo anayeaminika kutoka Gabon alihitaji matibabu ya dharura.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 kutoka Morocco alijaribu kumuingiza Cueta, lakini maafisa wa uhamiaji walimuagiza kufungua sanduku lake ambalo lilikuwa limefungwa katika kitoroli.
Kisa hicho kinajari wakati ambapo kumekuwa na jaribio la wahamiaji wengi kuvunja ua wa mita sita unaogawanya Cueta na Morocco.
Hakuna aliyefanikiwa kupita ,lakini watu wawili walijeruhiwa walipokuwa wakivunja ua huo na kupelekwa hospitalini huko Ceuta.
Mlinzi mmoja alipoteza jicho lake kulingana na maafisa.
Kisa kama hicho mnamo tarehe 9 Disemba kilihusisha zaidi ya wahamiaji 400 kutoka Afrika.
Melila- nchini Uhispania pia ni eneo jingine linalolengwa na wahamiaji.
Sign up here with your email