MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NI MAZIWA BORA – WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA - Rhevan Media

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NI MAZIWA BORA – WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA

aASSSSS

Mkurugenzi  wa  kampuni ya  Asas Bw  Salim Abri akiteta  jambo na  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Asas  akimweleza  jambo  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  Mkuu Kasim Majaliwa akifurahi jambo na Bw Asas
Viongozi  mbali  mbali  wakimsikiliza  waziri mkuu
Waziri  Mkuu  akitoa maelezo kwa  viongozi wa  mkoa  wa Iringa
Familia  ya Asas  wakifuatilia  hotuba ya  waziri mkuu
Mkurugenzi  mtendaji  wa kampuni ya  maziwa  ya  Asas Bw  Fuad Abri akisoma  taarifa ya  kampuni  hiyo  mbele ya waziri mkuu
Wananchi wakifuatilia  hotuba ya  waziri mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi akizungumza  mbele ya  waziri mkuu
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akifuatilia taarifa ya kampuni ya  Asas ,wengine ni salim Abri na Waziri  wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi
Farasi  waliopo shamba  la mifugo  la Asas
Askari  wa  FFU  Iringa  wakitazama ng’ombe shambani kwa  Asas
Nyati  wanaofugwa  shambani kwa Asas Iringa
Kundi  la  Nyati  wanaofugwa  shambani kwa Asas eneo la  Igingilanyi  Iringa
Askari  wa  FFU  Iringa  akipiga  picha na nyati waliopo  shambani kwa Asas
Asakari  wa FFU  Iringa  wakitazama vifaa  vya  kuhamilishia ng’ombe
Ng’ombe  waliopo  shamba la Asas   la  Nduli
Msafara  wa  waziri  Mkuu  ukiondoka  shambani kwa  Asas
Waziri  mkuu  akishukuru kwa   wenyeji kabla ya  kuondoka
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akiagana na  Salim  Abri
Waziri  mkuu akiagana na  mkurugenzi wa kampuni ya maziwa  ya  Asas  Fuad Abri
Waziri  mkuu  akitembelea  shamba  la mifugo  la Asas
Bw  Feisal  Abri  akimpa  maelezo  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  mkuu  akiendelea  kutembelea  shamba  la mifugo la Asas
Waziri  mkuu  Kasim Majaliwa  akitazama ng’ombe  ambao  wanasubiri  kupandikizwa mbegu
Zoezi la  kuhamilisha  ng’ombe  likifanyika
Mtaalam  akionyesha  namna ya  kupandikiza mbegu ng’ombe
Waziri  Lukuvi  kulia  akiteta  jambo na waziri  mkuu
Mtambo  wa  maziwa
Waziri  mkuu  akifurahi majina ya ng’ombe  za  Asas
Zoezi la kukamua  maziwa  likiendelea
Waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akisalimiana na Salim Asas  baada ya  kufika  kutembelea  shamba la mifugo  katikati ni mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza
Waziri mkuu  Kasim  Majaliwa na  viongozi  mbali mbali  wakielekea  kutembelea shamba la mifugo ya  Asas( picha na MatukiodaimaBlog)
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI  mkuu Kasim
Majaliwa amepongeza  kampuni ya maziwa
ya  Asas
Dairies Limited kwa  uzalishaji wa
bidhaa bora  nchini  na
kuwa ni kampuni pekee  ambayo
inafanya  vizuri  katika utengenezaji wa bidhaa bora za maziwa
na kuwa  imeweza kutekeleza kwa  vitendo kauli
mbiu ya  Rais Dkt  John Magufuli
ya Tanzania  ya  viwanda .


Kuwa  serikali  itaendelea
kuiunga  mkono kampuni  hiyo ya
Asas  ambayo pamoja na  kufanya
vizuri katika ubora  wa  maziwa
bado   ni  kampuni yenye sifa nzuri ya  ulipaji wa
kodi nchini  pia  ni kapuni ya mfano kwa  ufugaji bora
wa ng’ombe


“ Nimefurahishwa na ufugaji
bora  ufungaji  wa
mifugo   unaofanywa na Shamba la kampuni
ya Asas ya mkoani mkoani Iringa  ni  mzuri
sana lazima   wafugaji wengine
nchini  kufika kujifunza jinsi ya ufugaji
.”
Alisema
kuwa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya Asas Dairies kama  mtindi
unaozalishwa na kampuni hiyo ya  Asas ni mzuri  na hata  ukinywa hauna
hofu ya kuharisha kama mtindi inayotengenezwa na wengine 


Akizungumza leo
wakati wa ziara  yake ya  kutembelea
shamba la Asas lililopo eneo la Igingilanyi  katika
wilaya ya  Iringa ,waziri  mkuu
alisema  kuwa amefurahishwa na
ufugaji  unaofanyika katika  eneo hilo na kutaka   watu
wengine  kuanza  kufuga mifugo badala ya  kuwa
wachungaji wa  mifugo .


Kwani  alisema tatizo
kubwa ya  migogoro  kati ya
wachungaji na  wakulima
inasababishwa  na baadhi ya  watu kuendesha  uchungaji
wa mifugo  badala ya  kufuga
na  hivyo  kupelekea kugombea maeneo ya kuchungia
huku  wakulima   wakivamiwa na wachungaji hao .


Alisema  kwa  lengo la
kukomesha  migogoro  kati ya
wachungaji na   wakulima  anawaagiza
maofisa  mifugo  kote nchini
kuanza  kuitambua  mifugo
yote na  kuiweka alama  maalum
itakayosaidia  kutambua eneo  ambalo
mifugo  hiyo inatoka na  itakuwa ni njia ya  kukomesha wachungaji  kuhama hama 


Hivyo  alisema  ni
mhimu  sana  kwa
maofisa  Mifugo  katika Halmashauri  zote nchini
kuanza  kutoa  elimu kwa
wafugaji  ili kuondokana na  kuwa
na  mifugo mingi  isiyo bora
na  badala yake  kuachana na uchungaji  wa
mifugo  na  kujikita na ufugaji .


Alisema  kuwa  kwa
upande  wa Halmashauri  za
wilaya  zote  nchini
zinapaswa  kuwapimia  na kuwapa
hati ya umiliki  wa  ardhi
wawekezaji  wote  wakubwa
waliopo katika maeneo yao
lengo  likiwa ni  kuondokana na migogoro ya  ardhi .
Previous
Next Post »