MATOKEO KIDATO CHA NNE , SHULE ZA SERIKALI HOI - Rhevan Media

MATOKEO KIDATO CHA NNE , SHULE ZA SERIKALI HOI


MATOKEO ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka jana (2016) yametolewa leo ambapo shule za serikali zimeendelea kufanya vibaya huku zile za binafsi zikipeta,
Katika matokeo hayo jumla ya wanafunzi 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu ambapo madaraja yanayohesabika kama ufaulu ni kuanzia daraja la kwanza mpaka la nne.
Miongoni mwa shule kumi zilizoongoza hakuna shuke yoyote inayomilikiwa na serikali. Shule ya Feza Boys imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na St. Francis Girls, Kaizirege Junior na Marian Girls huku Marian Boys ikishika nafasi ya tano.
Matokeo hayo pia yanaonesha kuwa wavulana wamefaulu kwa asilimia 73.26 huku wasichana wakifaulu kwa asilimia 67.06.
Katika hatua nyingine, shule sita kati ya kumi za mwisho zimetoka katika Jiji la Dar es Salaaam.
Shule hizo ni pamoja na; Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Somangila, Mbondole na Kidete ambazo ni za serikali.


Previous
Next Post »