MADAKTARI WAPEWA SIKU 5 KUMALIZA MGOMO KENYA - Rhevan Media

MADAKTARI WAPEWA SIKU 5 KUMALIZA MGOMO KENYA

Madaktari na wauguzi wamekuwa wakigoma tangu mwezi DisembHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMadaktari na wauguzi wamekuwa wakigoma tangu mwezi Disemba
Mahakama nchini Kenya imewapa madkatari wa wauguzi muda wa siku tano kumaliza mgomo wao.
Maafisa wa chama cha madaktari walikuwa wamepewa vitisho kuwa watafungwa ikiwa mgomo huo haungeisha leo.
Madaktari wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara.
Wamekataa mshahara walioongezewa na serikali wa asilimia 40 wakisema kuwa ni wa chini kuliko ule walioafikiana mwaka 2013.
Karibu madaktari na wauguzi 5000 kutoka hospitali 2000 za umma, walianza mgomo wiki ya kwanza ya mwezi Disemba na wagonjwa wamekuwa wakikosa matibabu.
Jaji katoka mahakama ya ajira amesema kuwa siku hizo tano sio za mazungumzo bali za kumaliza mgomo.
Previous
Next Post »