LUKUVI KUGAWA HATI 800 KWA WANANCHI WA IRINGA - Rhevan Media

LUKUVI KUGAWA HATI 800 KWA WANANCHI WA IRINGA

LUKI


 Mji wa Iringa ukionekana kwa mbali
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (mwenye suti nyeusi) akitatua moja ya mgogoro wa ardhi mkoani Iringa.LUKI 1
………………LUKI 2
Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambapo jumatano hii tarehe 25 Januari 2017 atawapatia wakazi wa kijiji cha Kinywang’anga Iringa vijijini.
Katika ziara hii Mhe. Lukuvi atakutana na wananchi hao waliopimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba ambao kwasasa hati zao za umiliki wa ardhi hizo zimeishaandaliwa na  ziko tayari kukabidhiwa kwao.
Ziara hii ni katika utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi wenye lengo la kufanyika kwa nchi nzima. Utekelezaji huo utahusisha kuhakiki mipaka ya Mitaa na Vijiji pamoja na maeneo  mengine yote nchini na kupima kila kipande cha ardhi kwa lengo la kumilikisha ardhi hiyo kwa wananchi, taasisi na Kampuni.
Sambamba na hilo, Matangazo ya Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, Wilaya, Hifadhi za Taifa na vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote nchini kuhakikiwa na kukamilika.
Aidha mpango huu unalenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika kupanga, kupima, na kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za vipande vya ardhi ili kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Serikali ya awamu ya tano imeweka adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo sasa na kuzuia kasi ongezeko la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano kwa kuandaa mpango kabambe wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na mashamba.

Previous
Next Post »