KUKOSEKANA UZIO SHULE YA MSINGI MCHANGANYIKO PONGWE KUNA WEZA KUSABABISHA HATARI KWA WANAFUNZI. - Rhevan Media

KUKOSEKANA UZIO SHULE YA MSINGI MCHANGANYIKO PONGWE KUNA WEZA KUSABABISHA HATARI KWA WANAFUNZI.




WATOTO wenye ulemavu wa ngozi na wasioona wanaosoma shule ya msingi ya mchanganyiko ya Pongwe iliyopo Jijini Tanga wapo hatarini kuvamiwa na watu waovu na kuwafanyia vitendo vya kikatili kutokana kukosa uzio na sehemu kubwa kuzungukwa na pori ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Shule hiyo ambayo inapokea watoto wenye matatizo hayo kutokana mikoa mbalimbali Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana uzio huku sehemu kubwa ikipakana na pori jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa ustawi wao kielimu.

Hayo yalibainishwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Waziri Mfaume wakati wa ziara ya Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi aliyoifanya kuangalia changamoto ambazo zinaikabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Waziri alisema licha ya kufanya jitihada kubwa za kuanza ujenzi wa
uzio huo eneo la mbele ya shule hiyo lakini mpaka sasa hakuna msaada wowote ambao wamekuwa wakiupata ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linatishia usalama wa watoto hao.

Alisema awali changamoto hiyo ilikuwa eneo la mbele ya shule hiyo na kuona namna ya kulipatia ufumbuzi haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuwavutia wadau kuweza kusaidia lakini suala hilo mpaka sasa limeshindwa kupatiwa tiba.
Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi akiangalia namna wanavyoandika wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi ya Mchanganyika Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake 
Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wa kwanza kushoto akisikiliza kero za wanafunzi hao.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Mchanganyiko ya Pongwe ya wanafuzi wasiosikia na wenye matatizo ya ngozi (Albino),Waziri Mfaume kulia akimuonyesha diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi maeneo yenye mapori yaliyozunguka shule hiyo ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hao wakati wa ziara ya diwani huyo.

Previous
Next Post »